Wakati msimu wa Siku Kuu ukiwa unazidi kunoga, wasanii wa Bongo Movie wanazidi kuirudisha sanaa ya filamu kwenye ramani kwa kuonyeshwa filamu hizo kipindi hiki cha Siku kuu, kupitia TV Stations za kwenye ving’amuzi nyumbani kwako.
Filamu hizo za kibongo zimeanza kuonyeshwa wiki iliyopita ikiwa ni katika jitihada za makusudi za kuiweka Bongo Movie katika chati nzuri na kutazamwa na watanzania wengi wanaopenda kufatilia filamu za nyumbani pamoja na nchi za jirani.
Alhamisi hii saa 3:40 Usiku kupitia ST Swahili channel filamu ya ‘Umuhimu Wako’ inayowakutanisha Rose Ndauka, Yvonne Cherry (Monalisa) na Mama Natasha (Natashamamvi) itakuwa ikiruka kwa mara ya kwanza.
Filamu hiyo inahusu binti mmoja na kijana wa kiume lakini kila mmoja wao ana safari na historia tofauti ambayo ameipitia maishani mwake. Kijana anapata misukosuko akijaribu kusimama tena baada ya mkewe kufariki na kumuachia watoto wawili.
Upande mwingine; binti anakumbana na changamoto kwa baba yake mzazi ambaye anamuona binti huyo kama muhuni, Wawili hawa wanaingia katika mahusiano huku wakikabiliana na changamoto zao. Baadaye wanatulia baada ya majirani zao kuwasaidia, wanaoana na kuishi maisha ya furaha.
Filamu nyingine zitakazoruka wikendi hii ni ‘Mjerumani’ siku ya Ijumaa na ‘Milioni 10’ siku ya Jumamosi, filamu hizi za vichekesho zimesheheni mastaa wa Komedi kama vile Ringo na Mau Fundi.
UTACHEKA:Vibe la Pierre, Mzee wa Likwidii alivyokata keki na kucheza