Kocha Maurizio Sarri na Unai Emery wako katika nafasi nzuri kwenye makundi yao na wala hawana presha ya matokeo kuelekea game ya mwisho wa hatua ya makundi ya UEFA Europa League, hivyo tutarajie upangaji wao wa vikosi kuwapumzisha wachezaji nyota.
Kikosi cha Chelsea kilichochini ya kocha Maurizio Sarri licha ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita tayari wameshajihakikishia kumaliza wakiwa vinara wa kundi L katika michuano ya UEFA Europa League.
Kocha huyo muitalia anatarajia kuwapatia nafasi wachezaji ambao huwa hawapati namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, huku kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard amesema wanahitaji kuachana na ushindi walioupata dhidi ya Manchester City na kuangalia mechi zijazo.
“Unahitaji kuangalia zaidi kile unachotakiwa kufanya. Sisi tunataka kushinda, tunafurahi tumeshinda mchezo uliopita na tunajiandaa na mchezo wa Alhamisi (dhidi ya MOL Vidi)”>>>Eden Hazard
Kwa upande wa kocha wa Arsenal, Unai Emery yeye ana Vijana zaidi ya 10 walio chini ya umri wa miaka 20 na huenda akawatumia hao katika mchezo wao dhidi ya Qarabag huko nchini Azerbaijan, kwa upande wa Mbawana Samatta akiwa na club yake ya KRC Genk watahitaji ushindi katika game dhidi ya Sarpsborg ili kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua inayofuata kwani Kundi lao hadi sasa wote (KRC Genk, Besiktas, Malmo na Sarpsborg) wana nafasi.
Kutoka Bundesliga klabu ya RB Leipzig ambayo msimu uliopita ilicheza kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, safari hii wanahitaji kushinda mchezo wao dhidi ya Rosenborg huku wakitegemea ndugu zao Red Bull Salzburg washinde jijini Glasgow dhidi ya Celtic ili wao wapite kirahisi.
Balaa lingine ni kwa klabu ya AC Milan ambao wanafunga safari hadi Ugiriki kuumana na Olympiacos, wakiruhusu kufungwa magoli 2 watakuwa mameaga mashindano, game hizo ambazo zitaoneshwa ST World Football zitaanza kuchezwa kuanzia saa 23;00 kwa saa za Afrika Mashariki.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe