Michezo

Luis Suarez ndio shujaa wa FC Barcelona usiku wa UEFA Champions League

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay anayeichezea FC Barcelona ya Hispania usiku wa October 2019 katika uwanja wa Nou Camp aliibuka shujaa wa mchezo dhidi ya Inter Milan wa UEFA Champions League hatua ya makundi baada ya mchezo wao wa kwanza kutoka sare ya 0-0  dhidi ya Borussia Dortmund.

Barcelona baada ya kurudi katika uwanja wao wa Nou Camp walianza vibaya kwa kujikuta wakiruhusu kufungwa goli la mapema na Inter Milan dakika ya pili kupitia kwa Lautaro Martinez lakini mambo hayakuwa mazuri kwa Barcelona hadi walivyoingia kipindi cha pili.

Luis Suarez ndio alikuwa mkuki wa sumu wa Inter Milan kwani alifunga goli la kusawazisha dakika ya 58 na kufunga goli la ushindi dakika ya 85 na kuufanya mchezo umalizike kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1, Lionel Messi akiibuka kidedea kwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi (6) kuliko mchezaji yoyote katika mchezo huo, Barcelona sasa wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point 4 katika kundi lao sawa na Dortmund ayeongoza wakati Inter Milan na Slavia Praha wakiwa na point moja moja kila mmoja.

Matokeo ya game za Champions League October 2 2019.

VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments