Michezo

Adhabu aliyopewa aliyesababisha Okwi kupoteza fahamu uwanjani

on

Moja kati ya matukio yaliyotokea katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba ni kitendo cha mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kudaiwa kuwa alipoteza fahamu baada ya kupigwa kiwiko na mchezaji wa Ruvu Shooting.

Okwi ambaye alipigwa kiwiko cha shingo na Mau Bofu wa Ruvu Shooting, Okwi akiwa kashika mpira mkononi inadaiwa kuwa alianguka chini na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa lakini hata baada ya fahamu kumrudia alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na Laudit Mavugo.

Muamzi wa game hiyo alimuonesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Mau Bofu lakini leo kamati ya saa 72 baada ya kukaa na kupitia ripoti za muamuzi, kupitia kwa afisa mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura wametangaza kumfungia Mau Bofu mechi tatu na faini ya Tsh 500,000/=

VIDEO: Okwi amedaiwa kupoteza fahamu uwanjani baada ya kupigwa kiwiko

Soma na hizi

Tupia Comments