Top Stories

GHANA: Wasiojulikana waiba majeneza

on

Watu wasiojulikana wameripotiwa kuiba majeneza mawili na kutokomea nayo kusikojulikana. Watu hao wanadaiwa kutenda kisa hicho katika duka la majeneza lililopo katika eneo la Kumasi mkoani Ashanti katika taifa la Ghana.

Muuzaji wa majeneza hayo ambaye ameonekana akilalamika kupitia video inayoendelea kusambaa mitandaoni bila kutaja jina, amesema wezi hao katika majira ya usiku walichana uzio wa nyavu aliokuwa ameuzungushia katika biashara yake na kisha kuingia na kutokomea na majeneza hayo.

Ingawa haijafahamika hasa ni wapi wanayapeleka majeneza hayo lakini imekuwa ni moja kati ya habari zilizozua gumzo nchini humo huku wengi waliyoiona video hiyo wakibaki midomo wazi.

INAHUZUNISHA MZEE ALIYEJIKATA NYETI ZAKE ILI AFE “MKE KANIKIMBIA, BUNDUKI INASHTUKA”

Soma na hizi

Tupia Comments