Leo May 1, 2018 Rais Magufuli amekataa ombi la kuongeza mishahara kwa wafanyakazi kama lilivyoombwa na TUCTA kwa maelezo kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maendeleo.
Akizungumza leo katika sherehe za Mei Mosi mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi amesema kuwa kwasasa fedha nyingi zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maendeleo.
“Kwangu mimi naamini ukijenga reli Standard Gauge ukibeba mizigo mingi utatengeneza pesa nyingi, tukipeleka pesa nyingi hospitalini vifo vya akina mama vitapungua, kwangu mimi ninaona hilo ni la msingi” -Rais magufuli
“Mwaka huu tutaendelea pia kutoa nyongeza ya kawaida ya mishahara ya mwaka, tunataka wafanyakazi wapate haki zao” -Rais Magufuli
“Mimi ninaona ni vyema tukachukua BILIONI 437 tukawape mikopo Wanafunzi wa Vyuo Vikuu badala ya kuzitumia kujiongezea mishahara.” -Rais Magufuli
“Nikisema nitaongeza hizo pesa mimi nitazitoa wapi? naogopa kusema uongo. Hata mimi napenda kupandishiwa mshahara lakini kwa hali halisi ya sasa hivi lazima niwaeleze ukweli” -Rais Magufuli
“Nawaahidi, kipindi changu cha urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara kwa wafanyakazi, kupandisha kwangu haitakuwa kwa shilingi elfu kumi, itakuwa ni kupandisha kwelikweli” -Rais Magufuli
LIVE: Majibu ya Rais Magufuli kuhusu ombi la kuongeza Mishahara na kupandisha madaraja
VIDEO: MWANAMKE AANGUA KILIO MBELE YA RAIS MAGUFULI LEO MAY 1 2018, JPM ATOA MAAGIZO… TAZAMA HAPA CHINI KWENYE HII VIDEO
VIDEO: ALIKIBA ALIVYOMVALISHA PETE MKEWE AMINA…. TAZAMA HAPA CHINI