Michezo

Kutoka Morocco Msuva kafunguka hali ya mdogo wake, atafanyiwa upasuaji?

on

Baada ya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva kumuombea ruhusu mdogo wake James Msuva katika club yake ya KMC na kwenda nae Morocco kufanyiwa vipimo vya afya na kupatiwa matibabu kwa jeraha lake la tatizo la nyama za paja.

Leo AyoTV imeongea na Simon Msuva kutokea Morocco ambaye amefunguka kuhusiana na hali ya James Msuva ambaye yupo huko kwa matibabu, Simon Msuva aliomba akampatie matibabu James kwa gharama zake baada ya kusumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.

“Kwa ufupi James anaendelea vizuri alianza matibabu kwa timu yetu na sasa hivi yupo tu nyumbani kapumzika, kingine alienda tu kucheki mguu wake katika vipimo vikubwa vya MRI amekutwa na tatizo sio dogo sala wala kubwa sana lakini Dr mkuu alipata hudhuru kidogo alisafiri anarudi ndani ya wiki hii Mungu akipenda ataangalia majibu ya MRI na kuamua kuwa atafanyiwa upasuaji au atapatiwa matibabu mengine”>>>Simon Msuva

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments