Michezo

Bayern Munich wanaileta hii shabiki anaangalia game uwanjani akiwa kitandani

on

Club ya FC Bayern  Munich ya Ujerumani kwa sasa inaanza utaratibu mpya wa kuboresha mapato katika club yao kupitia uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena, Bayern leo wametangaza kuingia mkataba wa ushirika wa kibiashara na Marriott International.

Imeripotiwa kuwa uwanja wa Bayern Munich kwa siku zijazo mashabiki watakuwa na uwezo wa kuangalia game uwanjani Live wakiwa kwenye vyumba vyenye vitanda na vitu mbalimbali kama wapo katika hotel kubwa vile.

Huduma hiyo ya kulipia tiketi ya kuingilia uwanjani itakuwa ni maalum na kutakuwa na tiketi za VIPkwa ajili ya huduma hiyo, shabiki anaweza kukata tiketi na kuingia katika chumba maalum ambacho anaweza akawa yupo kama kwenye hotel na anaangalia game kama kawaida huku akipata huduma mbalimbali za ki-VIP.

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments