Michezo

Sababu za Arsenal kwa nini walimuondoa Harry Kane katika academy yao

on

Moja kati ya stori zinazotrend mara kwa mara katika mitandao ya kijamii kuhusiana na staa wa club ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ni picha ya utoto ya staa huyo inayomuonesha akiwa na jezi za Arsenal na kuripotiwa kuwa alikuwa katika academy ya Arsenal kipindi hicho.

Harry Kane wa sasa

Mkurugenzi wa zamani wa Academy ya Arsenal Liam Brady amefunguka sababu za Arsenal kumuondoa Harry Kane katika Academy yao kipindi hicho na anaamini alifanya makosa, baada ya sasa amekuwa ni staa mkubwa na mshambuliaji tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Spurs.

Liam Brady

Kwa mujibu wa Liam Brady anasema waliamua kumuacha Harry Kane katika Academy yao akiwa na umri wa miaka nane kwa sababu alikuwa ni kibonge na hakuwa na muonekano wa kiwanamichezo wakati huo, hiyo ndio sababu yao Kuu ya kuamua kuachana na staa huyo kipindi hicho.

Kushoto ni Harry Kane enzi hizo

Kwa sasa Harry Kane amefikisha rekodi ya kufunga magoli 101 katika EPL na goli lake la mwisho amewafunga Arsenal weekend hii katika uwanja wa Wembley, kwa upande wa Brady yeye alikuwa mchezaji wa Arsenal kuanzia 1971-1980 na mwaka 1996-2014 aliajiri na Arsenal kama mkurugenzi wa academy ya Arsenal.

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments