Nafahamu kuna watu wa nguvu ambao wameshajionea mambo mbalimbali na kuzipata story nyingi zinazotrend duniani kote kupitia millardayo.com, basi na hii ikufikie pia ya Hotel 10 za gharama zaidi duniani mwaka 2017.
10: Park Hyatt Paris Vendome, Paris, Ufaransa – Dollar 15,000 kwa usiku mmoja
Jiji la Paris limeingiza Hotel mbili kwenye list hii ambapo Park Hyatt Paris Vendome ikiwa ya kwanza kati ya mbili hizo. Unaambiwa itakugharimu dollar 15,000 kulala usiku mmoja kwenye Hotel hii ambapo moja ya sababu ambazo watu wengi hupenda kufikia katika Hotel hii, ni ukubwa wa jiji la Paris ambalo wageni wengi wanapenda kulitembelea.
9: Four Seasons Hotel George V, Paris, Ufaransa – Dollar 15,500 kwa usiku mmoja
Four Seasons Hotel George V ni Hotel nyingine ya kifahari katika jiji la Paris kuingia kwenye list hii ikikamata nafasi 9 duniani kwa kuwa na gharama. Imejengwa muda mrefu lakini ina sifa ya kuwa imara na yenye kila aina ya starehe na burudani ambapo utalazimika kulipa dollar 15,500 kwa usiku mmoja tu.
8: Le Richemond, Geneva, Switzerland – Dollar 17,000 kwa usiku mmoja
Kama ilivyo kwa mji wa Paris, pia kuna hotel mbili katika list hii kutoka katika jiji la Geneva. Moja kati ya hizo ni hii Le Richemond ambayo inakamata nafasi ya 8. Ni moja ya Hotel za kifahari katika jiji la Geneva ambapo kutokana na uzuri na mvuto wake, mteja hulazimika kulipa dollar 17,000 kwa usiku mmoja.
7: Burj Al Arab Hotel, Dubai – Dollar 17,500 kwa usiku mmoja
Sio watalii tu pekee ambao wanapenda kutembelea jengo hili, bali hata matajiri wakubwa kutoka duniani kote wanapenda kufikia katika Hotel Burj Al Arab kufurahia kutokana na huduma na uzuri wa hotel hiyo. Unaambiwa mastaa wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaipenda sana Hotel hii hivyo kuwafanya waitembelee mara kwa mara na kuifanya kuwa maarufu katika mji wa Dubai. Wageni wanaofikia Burl Al Arab hulipa dollar 17,500 kwa usiku mmoja.
6: Ritz-Carlton Hotel, Moscow, Urusi – Dollar 17,500 kwa usiku mmoja
Ni moja kati ya Hotel kongwe zaidi ya kifahari duniani katika jiji la Moscow. Siku zote Ritz-Carlton Hotel imekuwa juu kutokana na uzuri wake na gharama zake. Imekuwa ikibuni vivutio mbalimbali na kuifanya watu wapende kuitembelea ambapo hulazimika kulipa dollar 17,500 kwa usiku mmoja.
5: Atlantis Resort Hotel, Dubai & Bahamas – Dollar 24,000 kwa usiku mmoja
Hotel hii sio inashangaza tu kwa kujengwa kwake katika eneo la bahari ambalo ufukwe wake umetengenezwa, bali pia ni moja kati ya eneo la ajabu na zuri la kifahari duniani. Unaambiwa ufunguzi wa Atlantis Resort Hotel ulikuwa wa kihistoria na gharama kubwa ambapo takwimu zake ni dhahiri kuwa ni sehemu ya gharama sana. Ni moja kati ya kivutio na Hotel yenye gharama katika mji wa Dubai ambapo utalazimika kulipa dollar 24,000.
4: President Wilson Hotel, Geneva, Switzerland – Dollar 31,500 kwa usiku mmoja
Hii ni Hotel ya pili kutoka jiji la Geneva katika list hii. President Wilson ni Hotel ambayo inakamata nafsi ya nne ambapo unaambiwa utalazimika kulipa dollar 31,500 kulala usiku mmoja kutokana na ubora wa huduma zake.
3: Four Seasons Hotel, Manhattan, New York – Dollar 32,500 kwa uski mmoja
Hotel ya Four Season iliyopo Manhttan katika jiji la New York, Marekani ni moja kati ya hotel zenye samani za kifahari ambapo unaambiwa katika mji huo ni kama kivutio kutokana na uzuri wa mandhari yake. Wageni wanaotembelea hutakiwa kulipa dollar 32,500 kwa usiku mmoja.
2: Palms Casino Resort Hotel, Las Vegas, Nevada – Dollar 38,000 kwa usiku mmoja
Hotel ya The Palms Casino Resort inakamata nafsi ya pili kwenye list ya Hotel zenye gharama kubwa duniani. Hii inatokana na kuwa matajiri wengi hupenda kufikia kwa ajili ya mchezo wa kamari. Mtu kulipa dollar 38,000 kwa usiku mmoja kwa ajili ya kustarehe sio tatizo kwake kwa maana wacheza kamari wengi wanaofikia hapo ni matajiri wakubwa duniani hivyo hufurahia.
1: The Grand Resort Lagonissi, Athens, Ugiriki – Dollar 47,500 kwa usiku mmoja
Hii ndiyo hotel ghali zaidi duniani ambapo unaambiwa kwa yeyote anayetaka kulala The Grand Resort Lagonissi iliyopo katika jiji la Athens Ugiriki atalazimika kuandaa dollar 47,500 kwa usiku mmoja. Uzuri wa Hotel hiyo, uzuri na ubora wa chakula chake, magari ya kifahari ya kutembelea na wanawake wazuri ni miongoni mwa vivutio ambavyo watu wengi maarufu na matajiri hupenda kutembelea katika Hotel hiyo.
VIDEO: Diamond alivyozindua Chibu Perfume, na bei yake je? Bonyeza play kutazama.
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE.