Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: TOP 10: Zijue Hotel 10 ghali zaidi duniani kwa mwaka 2017
Share
Notification Show More
Latest News
Morgan Heritage kuachia album wasanii 16 washirikishwa
March 23, 2023
Baada ya uchaguzi kufutwa Arusha, makada wawili wajitokeza kuchukua fomu yupo mbunge na kada gonga
March 23, 2023
Serikali yashauriwa kuongeza Bajeti ya Usimamizi wa Usalama na Afya nchini
March 23, 2023
Mohammed Hussein afunguka haya kuhusu kutoitwa kwenye timu ya Taifa, ‘Taifa Stairs’
March 23, 2023
DC Jokate Mwegelo awataka hili Wafanyabiashara Wilayani humo ‘Bei za Vyakula’
March 23, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Duniani > TOP 10: Zijue Hotel 10 ghali zaidi duniani kwa mwaka 2017
DunianiNyumba/ Mijumba

TOP 10: Zijue Hotel 10 ghali zaidi duniani kwa mwaka 2017

April 22, 2017
Share
6 Min Read
SHARE

Nafahamu kuna watu wa nguvu ambao wameshajionea mambo mbalimbali na kuzipata story nyingi zinazotrend duniani kote kupitia millardayo.com, basi na hii ikufikie pia ya Hotel 10 za gharama zaidi duniani mwaka 2017.

10: Park Hyatt Paris Vendome, Paris, Ufaransa – Dollar 15,000 kwa usiku mmoja

Jiji la Paris limeingiza Hotel mbili kwenye list hii ambapo Park Hyatt Paris Vendome ikiwa ya kwanza kati ya mbili hizo. Unaambiwa itakugharimu dollar 15,000 kulala usiku mmoja kwenye Hotel hii ambapo moja ya sababu ambazo watu wengi hupenda kufikia katika Hotel hii, ni ukubwa wa jiji la Paris ambalo wageni wengi wanapenda kulitembelea.

9: Four Seasons Hotel George V, Paris, Ufaransa – Dollar 15,500 kwa usiku mmoja

Four Seasons Hotel George V ni Hotel nyingine ya kifahari katika jiji la Paris kuingia kwenye list hii ikikamata nafasi 9 duniani kwa kuwa na gharama. Imejengwa muda mrefu lakini ina sifa  ya kuwa imara na yenye kila aina ya starehe na burudani ambapo utalazimika kulipa dollar 15,500 kwa usiku mmoja tu.

8: Le Richemond, Geneva, Switzerland – Dollar 17,000 kwa usiku mmoja

Kama ilivyo kwa mji wa Paris, pia kuna hotel mbili katika list hii kutoka katika jiji la Geneva. Moja kati ya hizo ni hii Le Richemond ambayo inakamata nafasi ya 8. Ni moja ya Hotel za kifahari katika jiji la Geneva ambapo kutokana na uzuri na mvuto wake, mteja hulazimika kulipa dollar 17,000 kwa usiku mmoja.

7: Burj Al Arab Hotel, Dubai – Dollar 17,500 kwa usiku mmoja

Sio watalii tu pekee ambao wanapenda kutembelea jengo hili, bali hata matajiri wakubwa kutoka duniani kote wanapenda kufikia katika Hotel Burj Al Arab kufurahia kutokana na huduma na uzuri wa hotel hiyo. Unaambiwa mastaa wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaipenda sana Hotel hii hivyo kuwafanya waitembelee mara kwa mara na kuifanya kuwa maarufu katika mji wa Dubai. Wageni wanaofikia Burl Al Arab hulipa dollar 17,500 kwa usiku mmoja.

6: Ritz-Carlton Hotel, Moscow, Urusi – Dollar 17,500 kwa usiku mmoja

Ni moja kati ya Hotel kongwe zaidi ya kifahari duniani katika jiji la Moscow. Siku zote Ritz-Carlton Hotel imekuwa juu kutokana na uzuri wake na gharama zake. Imekuwa ikibuni vivutio mbalimbali na kuifanya watu wapende kuitembelea ambapo hulazimika kulipa dollar 17,500 kwa usiku mmoja.

5: Atlantis Resort Hotel, Dubai & Bahamas – Dollar 24,000 kwa usiku mmoja

Hotel hii sio inashangaza tu kwa kujengwa kwake katika eneo la bahari ambalo ufukwe wake umetengenezwa, bali pia ni moja kati ya eneo la ajabu na zuri la kifahari duniani. Unaambiwa ufunguzi wa Atlantis Resort Hotel ulikuwa wa kihistoria na gharama kubwa ambapo takwimu zake ni dhahiri kuwa ni sehemu ya gharama sana. Ni moja kati ya kivutio na Hotel yenye gharama katika mji wa Dubai ambapo utalazimika kulipa dollar 24,000.

4: President Wilson Hotel, Geneva, Switzerland – Dollar 31,500 kwa usiku mmoja

Hii ni Hotel ya pili kutoka jiji la Geneva katika list hii. President Wilson ni Hotel ambayo inakamata nafsi ya nne ambapo unaambiwa utalazimika kulipa dollar 31,500 kulala usiku mmoja kutokana na ubora wa huduma zake.

3: Four Seasons Hotel, Manhattan, New York – Dollar 32,500 kwa uski mmoja

Hotel ya Four Season iliyopo Manhttan katika jiji la New York, Marekani ni moja kati ya hotel zenye samani za kifahari ambapo unaambiwa katika mji huo ni kama kivutio kutokana na uzuri wa mandhari yake. Wageni wanaotembelea hutakiwa kulipa dollar 32,500 kwa usiku mmoja.

2: Palms Casino Resort Hotel, Las Vegas, Nevada – Dollar 38,000 kwa usiku mmoja

Hotel ya The Palms Casino Resort inakamata nafsi ya pili kwenye list ya Hotel zenye gharama kubwa duniani. Hii inatokana na kuwa matajiri wengi hupenda kufikia kwa ajili ya mchezo wa kamari. Mtu kulipa dollar 38,000 kwa usiku mmoja kwa ajili ya kustarehe sio tatizo kwake kwa maana wacheza kamari wengi wanaofikia hapo ni matajiri wakubwa duniani hivyo hufurahia.

1: The Grand Resort Lagonissi, Athens, Ugiriki – Dollar 47,500 kwa usiku mmoja

Hii ndiyo hotel ghali zaidi duniani ambapo unaambiwa kwa yeyote anayetaka kulala The Grand Resort Lagonissi iliyopo katika jiji la Athens Ugiriki atalazimika kuandaa dollar 47,500 kwa usiku mmoja. Uzuri wa Hotel hiyo, uzuri na ubora wa chakula chake, magari ya kifahari ya kutembelea na wanawake wazuri ni miongoni mwa vivutio ambavyo watu wengi maarufu na matajiri hupenda kutembelea katika Hotel hiyo.

VIDEO: Diamond alivyozindua Chibu Perfume, na bei yake je? Bonyeza play kutazama.

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE.

You Might Also Like

Silent Ocean imetupitisha kwenye Masoko ya vifaa mbalimbali Dubai, tazama (video+)

PICHA 10:Unahitaji Nyumba au kupanga Mikocheni, Palm Village wana habari njema

Forbes wamtangaza Melinda alieachana na Bill Gate kuwa Bilionea mpya, ashika namba hii

Picha za visiwa 10 vizuri zaidi duniani

Utafiti: Kuanzia miaka 55 watu wengi huchukia ajira zao….sababu?

TAGGED: duniani, majumba, Top 10
Admin April 22, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article AyoTV MAGAZETI: Mahakamani kisa kuflash simu, AG aruhusu viongozi kufikishwa Kortini
Next Article Majiji 10 yenye mvuto zaidi Afrika, imetajwa pia East Afrika
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Morgan Heritage kuachia album wasanii 16 washirikishwa
Entertainment March 23, 2023
Baada ya uchaguzi kufutwa Arusha, makada wawili wajitokeza kuchukua fomu yupo mbunge na kada gonga
Top Stories March 23, 2023
Serikali yashauriwa kuongeza Bajeti ya Usimamizi wa Usalama na Afya nchini
Top Stories March 23, 2023
Mohammed Hussein afunguka haya kuhusu kutoitwa kwenye timu ya Taifa, ‘Taifa Stairs’
Sports March 23, 2023

You Might also Like

Sports

Simba SC waingia Mkataba na MobiAd

March 23, 2023
Sports

Simba yaandika historia Ligi ya Mabingwa Afrika

March 22, 2023
Sports

Sheria Ngowi kutengeneza jezi za Zanzibar Heroes kwa miaka mitano

March 18, 2023
SportsTop Stories

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

March 17, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?