Habari za Mastaa

DMX kuipiga mnada nyumba yake ili kulipa deni linalomuandama

on

Inaripotiwa kuwa Rapper DMX ameamua kuweka sokoni nyumba yake aliyoinunua mwaka 2000 yenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 1 za Kitanzania ($649,000) na aliipata alipokuwa akifanya vizuri kwenye game ya muziki wa Hip Hop.

Inaelezwa kuwa nyumba hiyo ambayo ipo Mount Kisco mjini New York itauzwa kwa bei ya punguzo hadi kufikia kuuzwa shilingi Bilioni 1.6 za Kitanzania ($699,000) na inatajwa kuwa rapper huyo anadaiwa zaidi ya shilingi Bilioni 3 za Kitanzania. Rapper DMX anajaribu kulipa madeni yake baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja kutokana na kosa la ukwepaji kodi.

DMX aliachiwa huru January 2019 baada ya kukaa jela miezi 12 kwa kukutwa na hatia ya ukwepaji kodi na kudaiwa kiasi cha zaidi ya dola milioni 1.7, sasa moja ya masharti ya kuachiwa yalikuwa ni lazima alipe kiasi hicho cha pesa.

AUDIO: ULIPITWA NA HII YA NANDY KUMLILIA TENA RUGE? “NAKUMBUKA HII SIKU ULINISTUKIZA” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments