Michezo

Pogba kaulizwa kuhamia Real Madrid, jibu alilotoa ndio hili ….

on

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane baada ya kurejea katika club hiyo kutokana na kuondoka kwa miezi 9, ameanza kukisuka upya kikosi chake hicho ambacho alitwaa nacho mataji matatu ya UEFA Champions League mfululizo, Zidane ameanza kwa kudaiwa kuhitaji wachezaji mbalimbali wenye majina ambao anamini watakuwa na mchango.

Zidane ambaye amerudi Real Madrid ambayo haina matumaini, amekuwa akihusishwa kuwahitaji wachezaji mbalimbali kama Sadio Mane wa Liverpool, Kyliane Mbappe wa PSG huku akitajwa kuwa anaweza kuwa amemuweka kwenye rada zake pia kiungo wa Man United Paul Pogba.

Paul Pogba amenukuliwa na ESPN kuhusina na ishu kama anaweza akaenda kucheza Real Madrid na ametoa jibu linalomuonesha kuwa yupo tayari kwa lolote “Siku zote nimekuwa nikisema hivi, Real Madrid ni ndoto ya kila mmoja ni moja kati ya club kubwa duniani, Zinedine ni kocha pale, hivyo pale ni ndoto ya kila kijana na  kila mchezaji”>>>Paul Pogba

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments