Michuano ya fainali za Kombe la Dunia 2018 inaendelea nchini Urusi mataifa 32 yakiendelea kupambana kuwania taji hilo, unajua kuna mengi ya kufahamu kuhusiana na fainali za Kombe la Dunia 2018 zinazoendelea nchini Urusi.
AyoTV imeongea na mkuu wa vipindi Clouds FM Shaffih Dauda ambaye ni miongoni mwa team ya watu 23 ya Clouds Media iliyopo Urusi kwa ajili ya Kombe la Dunia, Shaffih ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na fainali hizo.
Haya ni baadhi ya mambo sita aliyoyaeleza kama unaenda Urusi utakutana nayo:
1- Fan ID kila shabiki anatakiwa kuwa na FAN ID ambayo ndio ataitumia kama VISA ya kuingilia Urusi na atapata acces ya kutumia usafiri wa umma bure akiwa na Fan ID.
2- Tiketi huwezi kupata kwa sasa kama hujapata tiketi kwani zote zimemalizika, au ukihitaji kuuziwa kutoka kwa mtu mkononi utalazimika tiketi ya Laki saba ulanguliwe hadi Tsh milioni 3.
3- Hakuna sehemu mgeni unakatazwa kutembea kwa sababu ya usalama, mamlaka za usalama Urusi zimejipanga kikamilifu kuhakikisha raia wote wanakuwa salama katika kipindi cha fainali za Kombe la Dunia.
4- Nchi ya Urusi katika fainali hizi za Kombe la Dunia hadi saa imepokea raia wa kigeni milioni 10 na kati ya hao ni raia milioni tatu pekee ndio wamepata tiketi.
Zaidi unaweza bonyeza play kusikiliza.
FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018