Michezo

Rais wa Congo Felix Tshisekedi kamteua Kidiaba kuwa Waziri

on

Golikipa wa zamani wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Congo ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa timu hiyo Robert Kidiaba ameendelea kuwa na wakati mzuri katika kazi yake ya siasa ikiwa ni miezi kadhaa imepita toka ashinde Ubunge, Kidiaba sasa ameteuliwa na Rais wa Congo Felix Tshisekedi  kuwa waziri wa michezo wa taifa la Congo DR.

Kidiaba kwa sasa ni mbunge wa jimbo la mkoa wa Katanga baada ya kuchaguliwa hiyo ni baada ya kustaafu kucheza soka lakini pia ni kocha wa makipa wa TP Mazembe wa sasa, baada ya kutua Tanzania na kuulizwa ishu za Ubunge ameweka wazi kuwa ameamua kuwatumikia mahali alipotoka.

Rais wa Congo Felix Tshisekedi

Kwa sasa Robert Kidiaba ana umri wa miaka 43 na ameamua rasmi kuwa kocha wa magolikipa wa TP Mazembe aliyoichezea kwa muda wa miaka 14 toka alipoamua kujiunga na timu hiyo 2002 akitokea AS Saint LucKidiaba alistaafu kucheza soka 2016 na alikuwa kipa wa timu ya taifa ya Congo ila kuchaguliwa kwake kuwa waziri wa michezo wa Congo kunaweza kumfanya akaachana na kazi yake ya ukocha.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments