Wiki kadhaa zilizopita zilisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha msanii wa Bongofleva Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akionekana kurudi kwenye dawa za kulevya.
Taarifa zingine zilikuwa ni kuhusu kuwa Chid Benz alipelekwa Sober House ili kuanza matibabu ya kumweka sawa kutoka kwenye matumizi ya dawa za kulevya, sasa basi maswali mengi yaliulizwa na mashabiki baada ya kusambaa kwa picha ikionesha akiwa na mkali wa Hip Hop Nash Emcee studio za Kiri Records.
Sasa leo millardayo.com & Ayo TV imempata Producer Rash Don ambae ameyazungumza haya kuhusu Chid Benz ……>>>Nashukuru Mungu Chid Benz anaendelea vizuri na hapa studio kuna wimbo amefanya na Mr Blue & Matonya alikuja kuusikiliza kama nimeshamaliza kufanya mixing kwani aliufanya muda mrefu’- Producer Rash Don
‘Na pia tulikuwa na mipango ya kufanya wimbo mwingine ukielezea matatizo aliyoyapata na pia kuhusu Nash Emcee alikutana nae hapa studio na ndio maana akapiga nae picha kwahiyo Chid Benz yuko katika afya nzuri na yuko tayari kufanya kazi’- Producer Rash Don
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Producer Don akizungumzia maendeleo ya Chid Benz
VIDEO: ‘Makonda wewe ni shujaa ishu ya Dawa za Kulevya sio mchezo’ Mh: Temba, Bonyeza play hapa chini kutazama