Mix

Waziri Jafo amewataka viongozi Kutembelea miradi mbalimbali

on

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesisitiza Viongozi na watendaji kutembelea miradi ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo hayo ili miradi hiyo iweze kutekelezwa vizuri kama inavyotakiwa.

Waziri Jafo aliyasema hayo leo hii alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya DMDP wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo ya kikazi ya waziri wa TAMISEMI ni muendelezo wa kazi tokea kuanza kwa mwaka 2019 iliyoanzia Wilayani Chemba, Kilosa, Kibiti, Rufiji, na Temeke.

Katika ziara hiyo Jafo alifanikiwa kufanya ukaguzi wa barabara za DMDP katika Kata ya Buza, ujenzi wa kituo cha afya Buza, pamoja na soko la kisasa linalojengwa eneo la Makangarawe, katika ukaguzi huo Jafo alifurahishwa Sana na kazi nzuri inayo tekelezwa katika eneo hilo.

Ameagiza kituo hicho pamoja na soko hilo la kisasa likamilike kabla mwezi June mwaka 2019

Waziri Jafo anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia thamani ya fedha zilizotewa chini ya ofisi ya Rais TAMISEMI kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote Nchini.

ULIIKOSA HII YA WAZIRI JAFO KUHUSU DAR ES SALAAM HATUTATEMBELEA MAGARI BINAFSI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments