Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

“Nashangaa media kutoa coverage kwa wazee wanaowapinga MO na Manji”-Edo Kumwembe

on

Usiku wa June 11 2018 mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya club ya Simba SC Mohamed Dewji alitoa tuzo kwa wachezaji, viongozi wa Simba pamoja na wadau mbalimbali ikiwa kama sehemu ya kutambua mchango wao katika club ya Simba SC.

Tuzo za MO Simba Awards 2018 zilihudhuriwa na tu mbalimbali ikiwemo mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe ambaye baada ya kuhudhuria tuzo hizo, asubuhi ya June 12 kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe mrefu kwa watu wa soka.

“Shughuli ya Simba jana ilikuwa Class…nzuri sana…iliandaliwa katika kiwango cha juu sana…may be the best one katika club levels..iliendana na ukubwa wa jina lao…nyuma ya shughuli hii amesimama sterling MO”

“klabu kama klabu ingekuwa na mtihani kufanikisha kitu kama hiki…wakati wa changes katika klabu zetu umefika kwa ajili ya mambo haya kuwa na consistency… Simba na Yanga zinahitaji mabadiliko ya kudumu ya uendeshwaji”

“Nashangaa sana kwa media kutoa coverage kwa wazee wachache sana ambao wanawapinga matajiri kama MO na Yusuf Manji…kitu cha muhimu cha kuzua mjadala ni namna ya kuwakabidhi hizi timu na si eti kulalamika ‘tunauza timu”

“Wakati huo huo tunaendelea kushabikia akina Manchester Unite, Arsenal, Barcelona kwa nguvu wakati zinaendeshwa kwa mifumo hii hii tunayotaka kuwapa akina Manji watuendeshe…sitatoa coverage kwa mtu anayepinga changes, nitatoa coverage kwa mtu anayetaka kuelimisha jinsi ya kufanya changes!..kwa sasa changes”

VIDEO: Alichozungumza MO Dewji kabla ya kutoa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments