Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Guardiola amgeukia Toure “Alikuwa na siku 365 za kunieleza hisia zake”

on

Moja kati ya majina ya mastaa wa soka walioyochukua healines hivi karibuni ni kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea Man City ya England Yaya Toure, baada ya kuondoka Man City aliamua kufunguka na kueleza kuwa kocha Pep Guardiola anawabagua wachezaji wa kiafrika.

Toure alifika mbali zaidi na kueleza kuwa ubaguzi unaofanywa na Pep Guardiola huwezi kuutambua kirahisi kwani ni mjanja sana, Toure alisema siku ikitokea kwenye kikosi cha Pep Guardiola akapanga first eleven yake wachezaji watano wa kiafrika, basi atanunua keki kumpelekea kama zawadi kitu ambacho anasema hakiwezi kutokea.

Baada ya tuhuma hizo kusambaa Pep Guardiola akiwa mapumziko kwao Hispania alihojiwa kuhusiana na tuhuma hizo na kujibu kwa kifupi tu “Toure anajua mimi sipo hivyo  wewe unataka mimi nifanye nini nilikuwa pamoja na Toure kwa miaka miwili na alikuwa na siku 365 za kunieleza hisia zake, sio kitu muhimu kukizungumzia kwa sasa”>>> Pep Guardiola

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

Soma na hizi

Tupia Comments