Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa 2019/2020 Simba SC aliikaribisha Tanzania Prisons uwanja wa Uhuru kucheza game yao ya 9 ya Ligi Kuu wakati Prisons ikiwa ni mechi yao ya 10.
Game hiyo ilimalizika kwa 0-0 na Tanzania Prisons inaendelea kuwa club pekee ya Ligi Kuu ambayo haijafungwa hadi sasa, kocha wa Simba SC Patrick Aussems aliongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo.
“Simba ilijitahidi kucheza mpira dhidi ya timu ambayo iliamua kucheza mchezo wa kujilinda (Prisons) na kushambulia kwa kushitukiza, nafikiri kwa Tanzania hii ni timu ambayo imejipanga zaidi, sijashangazwa (matokeo) kwa sababu wamefanya kazi kubwa na kupambana”>>>Aussems
VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”