Upande wa mashitaka umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuuonya upande wa utetezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kushindwa kujitetea kwa mara tatu mfululizo.
Hatua hiyo inatokana na Wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa Wakili mwenzake, Reuben Simwanza ndiye aliyeandaa mashahidi na kwamba leo alishindwa kutokea kwa kuwa anaumwa.
Nkoko alidai atahakikisha anaandaa mashahidi ili itakapotokea wakili mmoja hayupo, mwingine aendelee na shauri.
Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai kuwa hawana pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini wanaomba mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kesi ya upande wa utetezi inaahirishwa.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi January 26, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa.
Masogange anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
Watuhumiwa wa ugaidi Arusha wavua nguo Mahakamani
Watu 7 kizimbani kwa kujiunganishia bomba la mafuta ya Dizeli