Habari za Mastaa

Bifu la Tiwa Savage na Yemi Alade nje nje

on

Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Tiwa Savage pamoja na Yemi Alade kuhusishwa kwenye bifu kwa muda mrefu lakini kwa upande wao hawakuwahi kukiri popote kuhusiana na tuhuma hizo.

Leo December 21, 2018 bifu hilo limeonekana kuwekwa wazi hii ni baada ya Yemi Alade kumtupia dongo Tiwa Savage kuhusiana na muonekano wake na kusema kuwa amekuwa akijibinua kwenye picha ili kupata muonekano mzuri hasa hasa muonekano wa makalio kuonekana makubwa.

Yemi Alade ameandika “Acha kuongeza makalio yako kwenye picha unajijua kuwa upo kama I jikubali ulivyo Ahh ahh, unawadanganya mashabiki wako juu na chini”

Tiwa Savage ameonekana kupokea dongo hilo kutoka kwa Yemi Alade na kumjibu kupitia page yake ya twitter na kusema kuwa hayuko kwenye vita ya makalio na hatokaa kumuhukumu mwanamke yoyote hata awe ana vitu fake.

AY KAFUNGUKA KUHUSU MWANA FA KUZINDUA BODY SPRAY YAKE MPYA

Soma na hizi

Tupia Comments