Michezo

Dar Youth Cup 2019, hii inawahusu watoto wenye umri wa chini ya miaka 9, 11 na 13

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa baraka ya kufanyika kwa mashindano ya Dar Youth Cup 2019 ambayo itafanyika November 2 2019 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, michuano hiyo itachezwa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

Mashindano ya Dar Youth Cup yatahusisha vijana wenye umri wa chini ya miaka 9, miaka 11 na miaka 13 ambapo watakutana kutoka timu mbalimbali za wachezaji wenye umri sawa, ili kuweza kugundua na kuendeleza vipaji vya soka vya Tanzania kwa kushirikiana na One Plus.

Timu zilizoalikwa katika mashindano hayo ni timu 20 kutoka maeneo na shule mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, kutokana na umri wa washiriki waandaaji wa mashindano hayo watatoa zawadi mbalimbali kama medali na makombe lakini sio zawadi za fedha, hata hivyo sio mchezo wa soka pekee kutakuwa na mashindano ya tennis na kuogelea.

Timu zitakazishiriki katika mashindano hayo ndio hizi.VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments