Habari za Mastaa

Ciara na Russell wafungua label ya muziki, wamsaini msanii wao wa kwanza

By

on

Mwimbaji Ciara pamoja na mumewe Russell Wilson wameanzisha rasmi label yao ya muziki ambayo itainua vipaji vya wasanii wadogo na tayari wamemtangaza rasmi msanii wao wa kwanza ambaye atakua chini ya record label yao.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ciara ameweka wazi jina la msanii huyo ambaye anatambulika kama Deandre na Ciara amefunguka kuwa kijana huyo ni mkali wa sauti na ni kijana ambaye anafuata kuitingisha dunia kwenye masuala ya muziki. Kampuni yao inaitwa West2East Empire na Record Label yao inaitwa Beauty Marks Entertainment.

“Kutana na Deandre, kijana mwenye sauti yake anayefata kwenye hii dunia, tunayo furaha kutangaza kuwa tumemsaini nyota kwenye kampuni yetu ya West2East Empire na Record label ya Beauty Marks Entertainment, karibu kwenye familia Deandrea” >>>aliandika Ciara 

VIDEO: VITUKO VYA SHILOLE MBELE YA SHAMSA “MWENZANGU YAMEMSHINDA SIWEZI KUMWAMBIA NG’ANG’ANA”

Soma na hizi

Tupia Comments