Michezo

Obi Mikel amethibitisha baba yake alitekwa saa nne kabla ya game vs Argentina

on

Mtandao wa Kwese.ESP.com umethibitisha kupata taarifa kutoka kwa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria John Obi Mikel kuwa baba yake mzazi alitekwa saa nne kabla ya kucheza mchezo muhimu dhidi ya Argentina Jumanne iliyopita.

Obi amethibitisha kuwa alipata taarifa za kutekwa kwa baba yake lakini watekaji walimpa onyo asimwambie mtu yoyote au mamlaka za usalama nchini Nigeria, kwani angefanya hivyo baba yake angeuwawa.

“Waliniambia kwamba wangemuua baba yangu kama ningetoa taarifa kuwa ametekwa kwa mtu yoyote au mamlaka za usalama”>>>Obi Mikel

Watekaji lengo lao kubwa lilikuwa ni kujipatia pesa kutoka kwa staa huyo kwani walimuagiza atoe dola za kimarekani 28000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 60 za kitanzania  ili wamuachie baba yake akiwa hai bila kumdhulu kwa chochote.

Baba yake Obi na dereva walikuwa safarini kutoka Jos kuelekea sehemu za kusini mwa Nigeria kwa ajili ya mazishi lakini walitekwa na baadae kufanikiwa kuokolewa na Polisi July 2 ikiwa imepita wiki moja toka taarifa za kutekwa kwao ziliripotiwe kwa familia.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments