Michezo

Manara katoa ufafanuzi Mkude kukosa game 2 Simba SC

on

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara kaeleza kuwa kukosekana kwa Jonas Mkude katika mechi mbili za Simba SC dhidi ya Singida na Mwadui hakuna kitu chochote zaidi ya Mkude kupewa ruhusa maalum ya mapumziko maalum na uongozi wa timu.

“Jonas alikuwa anaumwa na alipewa mapumziko rasmi na uongozi wa klabu baada ya taarifa zake kutolewa na madaktari wa timu ya taifa (Taifa Stars kuwa anatatizo) lakini karibuni atararudi hakuna tatizo lolote”>>> Haji Manara

Kama utakuwa unakumbuka vizuri toka Jonas Mkude arejee jijini Dar es Salaam akitokea Sudan katika majukumu ya timu ya taifa, amekosekana katika michezo miwili ya Simba SC dhidi ya Singida na Mwadui FC ila Manara kawatoa hofu kuwa kiungo huyo alipewa mapumziko.

CHANZO: Azam TV

VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete

Soma na hizi

Tupia Comments