Habari za Mastaa

Drake atengeneza cover ya simu yake kwa Tsh Milioni 927

on

Rapa Drake sio mgeni katika kupenda kumiliki vitu vya luxury lakini hii imechukua headlines kubwa kutokana na maamuzi alioamua kuyafanya, mara nyingi haishangazi ukisikia Drake kanunua ndinga jipya kwa gharama lakini leo ameripotiwa kununua cover ya simu yake kwa gharama kubwa.

Drake ameripotiwa na mitandao mbalimbali nchini Marekani kuwa ameweka oda ya kutengenezewa cover maalum ya Iphone yake yenye madini ya almasi, cover hiyo maalum aliyoweka oda drake itakuwa na nakshinakshi za madini ya dhahabu nyeupe na blue diamond gram 18 ambazo ni dola 400,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Milioni 927.

Staa huyo wa hit single ya ‘God’s Plan’ ameweka oda hiyo kwa moja kati ya sonara maarufu duniani wa masuala ya uuzaji vito vya thamani anayejulikana kwa jina la Jason Of Beverley Hills, waandishi wa Marekani wanadaiwa kuwa Drake ambaye anapenda kuwa updated kwa kumiliki simu mpya kila inapotoka atapata hasara kama kampuni ya Apple itatoa toleo jipya la simu ambalo huwezi kutumia cover lake la thamani.

“VALENTINE’S HAIWAHUSU WASIO OA AU KUOLEWA, ALIKUFA MTU” MTAALAM

Soma na hizi

Tupia Comments