Michezo

Mbappe amekamilika Pogba mchezaji wa YouTube

on

Staa wa Paris Saint Germain Kylian Mbappe ambaye kwa sasa yupo nchini Urusi akiitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 jina lake linazidi kuchukua headlines toka aifungie Ufaransa magoli mawili katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Argentina.

Mbappe amepongezwa sana kuwa na mchango mkubwa akiwa na Ufaransa kiasi cha wachambuzi wa soka kumsifia na kumkosoa mwenzake Paul Pogba na kumuita mchezaji wa YouTube ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka wamewahi mara kadhaa kumkosoa.

Mchambuzi wa masuala ya soka Eamon Dunphy, amemkosoa Pogba na kumsifia Mbappe kwa kusema “Mbappe ana heshima sana akiwa mchezoni na mtu tofauti sana na wachezaji wengine ana ubinadamu nimesikia pesa zake za posho World Cup anawapa wasiojiweza, Mbappe mchezaji wa kisasa na mzuri huwezi kumlinganisha na Pogba”>>>Eamon Dunphy.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments