Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo leo amefanya mkutano na waandishi wa habari sambamba na kutangazwa kwa mpinzani wake atakayepanda nae ulingoni November 29, Mwakinyo sasa atapambana na bondia Arnel Tinampay kutoka Philipines.
Bondia atakayepambana nae Mwakinyo anatokea Philines katika kambi ya Manny Pacquiao ni bondia namba 2 nchini Philipines baada ya Manny Pacquia hivyo Mwakinyo kwa sasa anapata nafasi ya kupamba na bondia mkubwa ambaye hajawahi kupoteza pambano kwa KO.
Pambano hilo litakalochezwa November 29 2019 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, linaweza kuwa pambano la Ubingwa au elimination, ila bado haijathibitika zaidi ya kutangazwa kuwa mapema mwezi November itajulikana, March 23 2019 Mwakinyo alimpiga bondia raia wa Argentina Sergio Gonzalez round ya tano kwa TKO.
VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA