Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Azam FC imeendelea kutest Mitambo Chamazi

on

Wakati huu wa kalenda ya FIFA club ya Azam FC imeendelea kuitumia vizuri mapumziko hayo mafupi ya Ligi, yaliofanyika kwa ajili ya kupisha michezo ya kirafiki ya kimataifa, Azam FC wao wameendelea kujifua kwa kucheza michezo ya kirafiki na leo waliwaalika African Lyon katika mchezo wa kirafiki.

Azam FC pia imetumia mchezo huo kuendelea kuimarisha utimamu wa mshambuliaji wao mpya raia wa Burundi Seleman Ndikumana ambaye kutokana na kukumbwa na majeruhi alikuwa hajaichezea timu yake mchezo hata mmoja zaidi ya leo kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki tokea amesajili.

Ndikumana leo amecheza japo hakufanikiwa kufunga katika ushindi wa Azam FC wa magoli 2-0 yaliofungwa na Iddi Kipagwile dakika ya 17 na Jose Mahundi dakika ya 30, hivyo mchezo huo Azam FC wameutumia kama kujaribisha mitambo yao kwa kumpa nafasi zaidi Ndikumana ambaye kwa sasa anatafuta fitness.

VIDEO: Shiboub kalipa kisasi cha Simba SC kwa Mashujaa Kigoma

Soma na hizi

Tupia Comments