Michezo

Pyramids FC ndio wapinzani wa Yanga kimataifa, wanasajili mchezaji mmoja Tsh Bilioni 20

on

Club ya Yanga SC leo imetangazwa kupangwa kucheza game ya play off ya michuano ya CAF Confederation Cup dhidi ya Pyramids FC ya Misri na ikifanikiwa kuitoa timu hiyo basi itacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara nyingine tena.

Yanga atacheza dhidi ya Pyramids FC akianzia nyumbani October 27 2019 uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini mchezo wa marudiano utachezwa November 3 2019 nchini Misri, baada ya kutangazwa kwa ratiba hiyo Pyramids FC ikionekana kama jina geni mtandaoni usajili wao ndio unatisha zaidi.

Pyramids FC ilianzishwa mwaka 2008 ikijulikana kwa jina la Al Assiouty kabla ya baadae kununuliwa na Al-Sheikh ndio 2018 ikabadilishwa jina na kuitwa Pyramids FC, kikosi hiko kinatajwa kufikia thamani ya Tsh Milioni 50 hiyo inatokana na kusajili wachezaji wakubwa kutokea Brazil wanaocheza Ligi Kuu ya nchini humo.

Pyramids haioni tatizo kutumia pesa na ipo tayari kutumia kiasi kikubwa cha pesa ili kukamilisha usajili, inadaiwa Al-Sheikh ambaye ni bilionea wa Saudi Arabia aliyewahi kuwa Rais wa Al Ahly ya nchini humo, anaiandaa timu hiyo kama mpinzani wa Al Ahly, Pyramids FC ilimsajili Keno kutoka Parmeiras ya Brazil kwa dola milioni 10 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 20.

VIDEO: Uamuzi wa Simba SC kuhusu kudaiwa kugoma kwa Mkude, Erasto, Chama na Gadiel

Soma na hizi

Tupia Comments