AyoTV

Sababu za Yanga SC kuiondoa game yao na Pyramids FC uwanja wa Taifa

on

Ikiwa imepita siku moja toka shirikisho la soka Afrika CAF lichezeshe droo ya game za Play off za Kombe la shirikisho Afrika, huku Yanga SC ikipangwa kucheza dhidi ya Pyramids FC inayodaiwa kuwa na kikosi chenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 50.
Leo wametangaza maamuzi mazito kuhusiana na mchezo huo, awali game ilipangwa kuchezwa October 27 2019 na wengi walitegemea kuchezwa uwanja wa Taifa kama ilivyo kawaida ila Yanga SC wametangaza maamuzi tofauti.
Uongozi wa Yanga SC umetangaza kuwa mchezo wao huo wa kwanza nyumbani kabla ya kurudiana nchini Misri utachezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, AyoTV imeongea na Afisa muhamasishaji wa Yanga  Antonio Nugaz na ameeleza sababu za kuondoa mchezo huo uwanja wa Taifa.

VIDEO: Goli lililoipa Tanzania Ubingwa wa CECAFA U-20 dhidi ya Kenya

Soma na hizi

Tupia Comments