Michezo

Ujumbe wa mwisho wa Emiliano Sala kabla hajapotea

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa anaichezea club ya Nantes ya Ufaransa Emiliano Sala, alipotea kwa ndege yao binafsi aliyokuwa anasafiria kutoka Nantes kwenda Wales kuanza kuitumikia timu ya mpya ya Cardiff City.

Emiliano Sala mwenye umri wa miaka 28  alijiunga na Cardiff Jumamosi hii akitokea Nantes, hivyo ndege aliyokuwa amepanda Emiliano Sala akitokea Nantes kuwaaga wachezaji wenzake ilipotea usiku wa January 21 ikiwa katika pwani ya Guemsey, ila dakika chache kabla ya kuondoka Nantes, Emiliano alituma ujumbe katika group la whatsapp la wachezaji wenzake akieleza hofu ya ndege aliyopanda.

“Usiku wa jana nilikuwa Nantes na nimefanya vitu vingi sana na nimechoka kesho ni siku ya kuondoka na nimefanya mazoezi kitu cha kwanza kwa sasa nipo kwenye ndege naenda Cardiff ndege ambayo inaonekana kama itaanguka hivi, kama hutokuwa umesikia chochote kutoka kwangu kwa saa moja na nusu kutokea sasa sijui nini kitakuwa kimetokea wanatakiwa wamtume mtu kuja kunitafuta naogopa sana”>>> Emiliano Sala

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments