Club ya Chelsea imeamua kuvunja ukimya na kutoa taarifa rasmi kuhusiana hali za kiafya za wachezaji wake Mesut Ozil na Seadac Kolasinac baada ya jaribio la kuvamiwa na vibaka na kutolewa visu mapema leo katika jiji la London.
Ozil akiwa katika gari yake akiwa kaongozana na mchezaji mwenzake wa Arsenal Kolasinac alitolewa kisu na vibaka walimfuata na pikipiki kwa lengo la kutaka kumpora lakini ujasiri wa Kolasinac kushuka mikono mitupu na kutaka kupambana nao kulifanya jaribio hilo kufeli na kufanikiwa kumnusuru Ozil.
Vibaka hao walikuwa wamevaa wamesweta ya mikono mirefu huku wakiwa wamevaa kofia ngumu za pikipiki zilizokuwa na kioo cheusi (helmet) kwa lengo la kujificha lakini lengo lao halikutimia, kufuatia taharuki hiyo Arsenal wametoa taarifa rasmi kuwa Ozil na Kolasinac wapo salama hakuna aliyejeruhuiwa wala kuumia.
VIDEO: Mwanzo Mwisho Mzee Kilomoni wa Simba SC alivyofuatwa na Polisi na kuchuliwa