Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Olivier Giroud ameomba msamaha hadharani kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kufuatia kugundulika kwa usaliti kwenye ndoa yake.
Kwa takribani wiki moja sasa hivi kumekuwa na tetesi kwamba Mfaransa huya alimsaliti mkewe kwa kutoka na mwanamitindo Celia Kay likiwa ni tukio lililotokea usiku wa kuamkia mechi ya Arsenal vs Crystal Palace February 2 2014 hotelini London.
Gazeti la Sunday Sun lilikuwa la kwanza kuripoti taarifa hizo lakini Giroud alisema ni uongo, lakini jana gazeti hilo likatoa ushahidi wa picha ambayo inasemekana ilipigwa na Kay, ikiwa inamuonyesha Giroud akiwa kavaa nguo ya ndani wakiwa bado chumbani.
Mshambuliaji huyu wa kifaransa ambaye alikanusha taarifa hizo mwanzoni, hakuwa na jinsi tena zaidi ya kukiri kutokea kwa tukio hilo na kuamua kuomba radhi kupitia page yake ya twitter.