Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi, kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyodaiwa kufanywa na raia wa China wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro, Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni Watanzania.
Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita’– Mwigulu Nchemba
‘Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki,Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari– Mwigulu Nchemba
Unaweza ukabonyeza Play kumsikiliza Waziri Mwigulu Nchemba akimzungumzia raia wa China kufanya unyanyasaji huo Geita
ULIIKOSA HII YA MWIGULU NCHEMBA NA WASANII WA BONGOFLEVA ANAOWAKUBALI BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA