Video Queen Agness Gerald maarufu kama ‘Masogange’ ambaye ametokea kwenye video kadhaa za muziki wa Bongofleva, leo March 21, 2017 alikwenda Mahakamani Kisutu Dar es salaam kufuatia kuitwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa wakili wake aitwae Nictogen Itege ameiambia millardayo.com kuwa kesi imeahirishwa mpaka tarehe 20 mwezi April kwasababu upande wa Serikali bado haujakamilisha Upelelezi juu ya kesi ya Video Queen huyo.
‘Leo kesi ilikuwa mara yake ya mwisho kutajwa lakini imepangiwa tarehe nyingine ambayo imepangiwa tarehe 20 mwezi April kama alivyosema mheshimiwa kuwa Serikali bado hawajakamilisha upelelezi kwa hiyo hayo ndio naweza kukuambia kwa sasa’
ULIIKOSA HII YA AGNESS MASOGANGE ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI FEB 22, 2017 BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA