Habari za Mastaa

U HEARD: Maneno ya Q Chief kuhusu producer aliyevujisha wimbo wake na Patoranking

on

December 8, 2016 U Heard ya Clouds FM leo iko na stori kuhusu mwimbaji mkongwe Shaban Katwila a.k.a Q Chief/ Q Chillah ambaye amezungumza na Soudy Brown kuhusu kuvuja kwa wimbo wake mpya aliofanya na star Patoranking kutoka Nigeria.

Kwa mujibu wa Q Chief amesema kuwa wimbo huo umevujishwa na producer aliyeshiriki kutengeneza wimbo huo mwanzoni, na kwasasa hawana maelewano mazuri tangu alipoamua kumuongeza producer Abby Dady ili amalizie sehemu zilizobaki.

“Mzigo umevujishwa na watu ambao hawana upendo hajui maumivu ya mtu na hawatambui nini mtu amefanya, mimi nimesikia jana usiku na imeniumiza sana kwasababu tulitarajia kuachia wimbo huu mwezi January kwa mujibu wa kaka zangu, Huyu mtu ni kama alikuwa anasubiri nipost cover ili aone nini kitatokea.” – Q Chief

Kuipata full stori bonyeza play hapa chini kusikiliza.

 

VIDEO: Wapo hapa wasanii ambao Patoranking amefanya nao Collabo. Bonyeza play kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments