Top Stories

Trump atishia kufutia leseni vituo vya runinga Marekani…..sababu?

on

Rais Donald Trump ametishia kufungia vyomba vya habari bya Marekani leseni za kutokana na mgogoro unaoendelea baina yake na vituo vya runinga nchini humo akidai kuwa vimekuwa na upendeleo.

Trump alikasirishwa na ripoti ya kituo cha habari cha NBC iliyodai kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba anataka kuongezwa kwa kiwango kikubwa cha silaha za nyuklia nchini humo.

Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita bwana Trump ‘mtu mjinga’ matamshi ambayo Bwana Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameyataja kuwa habari bandia.

Ulipitwa na hii? YALIYOMKUTA MWALIMU ALIYETEMBEA NA MWANAFUNZI WAKE ROMBO

Soma na hizi

Tupia Comments