Michezo

Usisahau kuwa kocha wa Genk kampa dakika 75 Samatta leo, ushindi wao huko hapa

on

Usiku wa April 20 2016 kocha wa KRC Genk Peter Maes kaendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuanza katika first eleven yake nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea klabu hiyo Mbwana Samatta, Maes amempa nafasi Samatta ya kuanza mchezo wa pili mfululizo.

Licha ya kuwa KRC Genk walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Cristal Arena kukabiliana na vinara wa Ligi hiyo Club Brugge, Maes kamuamini Samatta na kumpa nafasi katika mchezo huo mgumu ulio malizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 4-2. Samatta amecheza kwa dakika 75 na dakika ya 76 alitoka akaingia Nikolaos Karelis.

sama 4

Samatta anakuwa amefikisha jumla ya mechi tatu alizoanza akiwa na KRC Genk katika mechi hizo amefunga mechi mbili goli moja moja katika kila mchezo, magoli ya KRC Genk ya leo yamefungwa na Onyinye Ndindi dakika ya 15, Alejandro Melero dakika ya 42, Thomas Buffel dakika ya 45 na Jeren Uronen dakika ya 73.

Screenshot_2016-04-21-01-14-18-1

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

GOLI LA PILI LA MBWANA SAMATTA AKICHEZA FIRST ELEVEN YA KRC GENK

Soma na hizi

Tupia Comments