Michezo

Goli la Ulimwengu la leta kizaazaa TP Mazembe, refa afungiwa

on

Club ya Sanga Balende ya Mbujimayi Congo DR baada ya mashabiki wao kufanya fujo na kuwapiga wachezaji wa TP Mazembe.

Belende wamepewa adhabu ya kucheza mechi zao tatu zijazo za Ligi Kuu Congo DR nje ya mji wao pamoja na faini ya USD 5000 ( huku kiongozi wao Mr Lumbala akifungiwa kwa miezi 24 kutoingia viwanjani.

Refa wa mchezo huo Kibingo Numbi na mshika kibendera namba 2 Mpaka Mayasi na wao wamefungiwa kwa kipindi cha miezi 24 kuchezesha soka.

Wachezaji na viongozi wa TP Mazembe walipigwa hadi kulazimika kupanda magari ya Polisi kuondoka uwanjani.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Balende walipoteza mchezo huo nyumbani kwa kufungwa 1-0 na TP Mazembe goli ambalo lilifungwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 94 ya mchezo.

Ulimwengu akiongea na AyoTV alieleza Balende walikuwa wakijiangusha kwa muda mrefu ikiwa ni mbinu ya kutaka sare.

Soma na hizi

Tupia Comments