Michezo

Golikipa wa Ivory Coast Badri anahitaji faraja kuliko kejeli

on

Golikipa wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast Badra Ali Sangare anapitia wakati mgumu, baada ya jana kuwa gumzo mitandaoni kwa kufanya kosa dakika ya 93 na kuwafanya Sierra Leone wapate goli lililofanya sare ya 2-2.


Mchezo huo ulikuwa ni muhimu zaidi kwa Ivory Coast na sasa wako kwenye hatari ya kufuzu au kutofuzu 16 bora ya AFCON 2021, Badri leo kaamka na taarifa za kufiwa na baba yake mzazi Toumani Sangare.

Madhara makubwa ya kosa alilolifanya yanakuja kutokana na kuwa mchezo wao ujao dhidi ya Algeria utakuwa kama fainali sababu ya wote watakuwa wanahitaji point wakati Algeria atakuwa anahitaji ushindi zaidi.

Soma na hizi

Tupia Comments