Club ya Man United imethibitisha kuwa golikipa wao Sergio Romero amepata ajali ya gari leo akiwa karibu na uwanja wa mazoezi wa Man United unaojulikana kama Carrington, Man United wamethibitisha kipa huyo hakupata majeraha yoyote yuko salama.
Kwa mujibu wa picha zilizokuwa zinaoenekana katika mitandao zinazonesha kuwa Romero amepata ajali akiwa kwenye gari yake binafsi aina ya Lamboghini yenye thamani ya pound 170,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 500.
Romero mwenye umri wa mika 32 amekuwa golikipa namba mbili wa Man United chini ya David De Gea, ambapo pia amekuwa na nafasi finyu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Man United.
VIDEO: Kinachoendelea Villa Park England muda huu, akisubiri kutangazwa Samatta