Mix

Good News kwa wafanyabiashara, ahadi yatolewa na Waziri Kitila

on

Serikali imeahidi kuendelea kujitolea kusaidia kuweka mazingira mazuri katika Viwanda na Makampuni ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakua.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo wakati akitoa Tuzo ya Wakurugenzi Bora 100 kwa Mwaka 2021 zilizoandaliwa na kampuni ya Eastern Star Consulting Group na kutolewa jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kwasasa serikai inaendeea kuweka mazingira mazuri yatakayofanya makampuni na viwanda viweze kufanya vyema ili kuweza kulipa kodi na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
“Niwapongeze wote miweza kushinda tuzo hizi na kufanikisha makampuni yenu kufanya vyema licha ya changamoto ya COVID 19, mliweza kumudu na kufikia maleng na mafanikio. Hili somo ni kubwa na mmethibitisha kuwa unapokuwa na uthubutu unaweza kukabiliana na changamoto hata wakati wa shida”>>> Prof Mkumbo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Eastern Star Consulting Group Bw.  Deogratius Kilawe ameyashukuru makampuni kwa kuweza kujitokeza kushiriki kimamilifu licha ya changamoto za hapa na pae zilizojitokeza.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo akimkabidhi mshindi wa Tuzo ya Wakurugenzi Bora 100 kwa Mwaka 2021 ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati). Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Eastern Star Consulting Group Bw. Deogratius Kilawe ambao ni waandaaji wa Tuzo hizo.

Tuzo hizo ni mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania hivyo ameyamba makampuni na viwanda kujitokeza kwa wingi mwaka 2022.

Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (Wapili toka kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj (Wakwanza toka kulia) na wengine.

Soma na hizi

Tupia Comments