Gosberth Kibanza aka Gosby msanii wa kizazi kipya mwenye hit mbalimbali kama Monifere na Video yake ya BMS ambayo ilivuka mipaka mpaka kituo cha channel O ya Afrika Kusini amekuwa msanii wa kwanza wa kizazi kipya kuwa accepted na VEVO na kumpa account ya kuweka kazi zake za kimuziki.
VEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video za music na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal Music Group, Warner Music Group na Google ,VEVO ni mtandao number moja duniani unahusika na kuhifadhi na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu duniani, kama Jay Z, D’banj, Nick Minaj, Mafikizolo na wengine wengi.
Msanii mwingine wa Tanzania ambae ana account ya VEVO ni Rose Muhando ambae anafanya kazi na Sony Afrika ambapo kuna stori kwamba ukiwa na account ya VEVO kuna baadhi ya malipo unapata pale matangazo yanapoonekana kwenye video yako.
Baada ya kupata Account hiyo ya VEVO Gosby amesema >>’Nina furaha kubwa sana kwa kuwa mara nyingi nimekuwa natamani kuwa na account ya VEVO, VEVO ni platform kubwa ya wasanii na wadau wa muziki duniani’
‘Nafurahi kuwa miongoni mwao sina shaka kazi zangu zitatazamwa na wadau wakubwa wa soko la muziki afrika na dunia,yah unaweza kuwa na video zako youtube kama wanamuziki wengine au hata wasio wanamuziki lakini VEVO ni maalum kwa Established Musicians Only’
‘Hata mtu akitazama Music Video zako VEVO anakuwa na uhakika kuwa hii ni video ya Established artist, nadhani ni njia iliyosahihi kwa wanamuziki wa kizazi kipya hapa nyumbani kujaribu kupata VEVO accounts’
‘Wenzetu wa Afrika Magharibi na Afrika Kusini wanamuziki wao wote wakubwa wana VEVO accounts, mapinduzi yetu ya muziki yasiishie kwenye platform za hapa nyumbani tu, tutumie fursa zaidi za masoko na kujitangaza kwenye mitandao mikubwa duniani’
‘Imeichukua management yangu takribani mwezi mmoja na zaidi kufuatilia, kujaza form na mwishowe kuwa accepted na VEVO inayopatikana kwenye Youtube.com na VEVO.COM, nichukue fursa hii kuipongeza management yangu kwa kazi nyingine bora na yakujivunia na vile vile nitumie fursa hii kuwapongeza mashabiki wangu kwa uvumilivu waliokuwa nao katika kipindi hiki cha ku-migrate kazi zangu kutoka youtube na kwenda VEVO ‘
‘video yangu ya BMS ilikuwa na Views 45,000 kipindi tunaishusha ili kuweza kuhamia VEVO ikiwa ni moja ya masharti ya VEVO ili kuzuia uzagaaji holela wa kazi”
Gosby pia ameongelea wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni aliomshirikisha Ommy Dimpoz >>’Yeah nina kazi nyingi ambazo ziko kwenye studio tofautitofauti ambazo nimefanya na producers tofauti tofauti kama 10 hivi na zimefanywa na producers tofauti kama 7 wa hapa nchini na nje ya nchi’.