Top Stories

Grace anaedaiwa kumuua mpenzi wake akamatwa

on

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Grace Mushi maarufu mtaani kwao kwa jina la Neema kwa tuhuma za mauaji ya mpenzi wake Hamis Abdallah ‘Zungu’ ambaye alimmwagia Petroli akiwa ndani kisha kumchoma moto.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Mbezi Makabe kwa Mzungu.

“Muda wa saa 8:30 usiku Mtuhumiwa huyu alimfungia ndani ya nyumba Hamis akammwagia mafuta ya Petrol na baadaye akachoma moto kitu kilichosababisha Hamisi kufariki” Kamanda ACP Muliro Jumanne Muliro.

“Hamis alikua ni Rafiki yake wa kiume (Boyfriend), Mtuhumiwa alijaribu kutoroka lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi tukamkamkata na uchunguzi umebaini kulikuwa na mgogoro mkubwa wa kimapenzi kabla kufanyika kwa tukio hili la Kikatili” ——— Kamanda ACP Muliro Jumanne Muliro.

DIAMOND PLATNUMZ AAGIZA LAMBORGHINI NA BENTLEY, MAGARI YA MABILIONEA

Soma na hizi

Tupia Comments