Mix

Kumbe Tuzo za Grammy Awards hutolewa hata kwa Marais pia! Marais hawa 3 walishawahi kuzipokea..

on

THE THREE

Kwenye picha ya pamoja ni Barack Obama, Michelle Obama , Jimmy Carter na Bill Clinton.

Wengi tunazijua tuzo za Grammy Awards ambazo hutolewa kila mwaka Marekani kama Tuzo za pongezi kwa wale wote waliofanya kazi nzuri kwenye industry ya Entertainment kwa mwaka husika.

Lakini Tuzo za Grammys hutolewa hata kwa viongozi wa Siasa pia, hapa nazungumzia Marais na watu wengine kwenye taaluma nzima ya Siasa… inawezekana ulikuwa unajua au hujui, lakini Tuzo hizi hutolewa chini ya category ya Grammy Award for Best Spoken Word Album.

obama2

Barack Obama

Category ya Grammy Award for Best Spoken Word Album ni Tuzo inayotolewa kwa wale watunzi wa mashairi, waandishi wa hadithi na watunzi wa vitabu vya sauti (audio books) na mara nyingi tuzo hizi hutolewa tofauti ili kulinda heshima ya watu husika.

JIMMY

Jimmy Carter alikuwa Rais wa Marekani mwaka 1977hadi 1981.

Baadhi ya viongozi waliowahi kupokea tuzo hii ni Marais wa 3 wa Marekani, Jimmy Carter, Bill Clinton na Barack Obama. Watu wengine waliowahi kupokea tuzo hiyo pia ni Senetors 4, Everett Dirksen, Hillary Clinton, Barack Obama (alikuwa Senetor wa Illinois) na Al Franken.

Bill Clinton during Bill Clinton Presented with His GRAMMY Award for Best Spoken Word Album for "My Life" - February 17, 2005 at Green Acres in Beverly Hills, California, United States. (Photo by L. Cohen/WireImage for The Recording Academy (View ONLY))

Bill Clinton alikuwa Rais wa Marekani mwaka 1993 hadi 2001.

Jimmy Carter alipokea tuzo hii mwaka 2007 kwa audio book yake ya Our Engaged Values, Bill Clinton mwaka 2005 na 2008 kwa My Life (audio book) na Giving (audio book) pamoja na Barack Obama 2007 na 2008 kwa Dreams From my Father na The Audacity of Hope vyote vikiwa audio books.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments