Watu wanaoishi Njoro Kaunti ya Nakuru, Kenya wameiomba Serikali ya nchi hiyo kuwasaidia eneo la kufanyia mazishi kutokana na uhaba wa ardhi.
Ishu ni kwamba kutokana na maeneo ya makaburi kutotosha watu wamejikuta wakilazimika kuchimba makaburi yenye vina vifupi juu ya makaburi mengine ili waweze kufanya mazishi.
“Serikali itupatie mahali ambapo tunaweza kuzika watu wetu kwa amani.. sio ukizika ukienda kulima unapata umefufua mtu mwingine… mnarudi mnamuweka pembeni hata yeye hilo kaburi lilinunuliwa ilipaswa na yeye aweze kuzikwa”– alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Ukosefu wa ardhi ya kuzikia ni taatizo kubwa linalokumba maeneo mengi nchini humo.
Nimekuwea sauti ya taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook