Mix

Ghalib Mohamed wa GSM atunukiwa tuzo ya ubora ya Mwaka

on

Kampuni ya GSM ni moja ya kampuni zenye sifa zake hapa Tanzania, tumeshuhudia bidhaa mbalimbali zikiwa na ubora chini ya nembo ya GSM mfano Pikipiki, AC, Mabati na hizo ni baadhi tu, kwa Dar es salaam kuna mpaka Mall za GSM ambako ndani yake kuna mkusanyiko wa maduka makubwa.

Ukitembelea GSM Malls Dar es salaam Msasani Road karibu na ubalozi wa Marekani au Pugu Road ndio utaelewa ninachosema na ndio maana Tanzania Leadership Awards wameamua kumtunuku Mwenyekiti wa GSM tuzo.

Ghalib Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa GSM Group Ltd. amepewa tuzo ya Mwenyekiti bora wa mwaka na ni baada ya kuona kazi kubwa iliyofanywa na GSM iliyo na project nyingi ndani yake lakini bado imebaki kuwa namba 1 kwa kuwahudumia Watanzania pamoja na kutoa misaada Tanzania kupitia Timu ya Madaktari iliyozunguka nchi nzima.

Unaweza kutazama kwenye hii video hapa chini kujionea moja ya kazi za GSM

Soma na hizi

Tupia Comments