Top Stories

UPDATES: Kuhusu ile kesi ya Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent

on

Ni Updates kuhusu kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent Innocent Mushi na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Nkana leo November 14, 2017.

Kesi hiyo imeshindwa kusikilizwa baada ya Hakimu kutokuwepo Mahakamani ambapo wanakabiliwa na mashtaka dhidi ya kuruhusu gari kubeba Wanafunzi bila kuwa na kibali, kuruhusu gari kutembea barabarani bila kuwa na bima, kushindwa kuwa na mkataba wa kazi na Dereva na kuzidisha abiria 13 kwenye gari lililokuwa limebeba wanafunzi.

Kosa linalomkabili Makamu Mkuu wa Shule hiyo Longino Mkana ni kuruhusu gari hilo kuzidisha abiria 13 ambapo baadaya Hakimu kukosekana Mahakamani leo kesi hiyo imeahirishwa hadi December 18, 2017.

ULIPITWA?? DR. LUIS SHIKA AONGEA BAADA YA KUTOKA POLISI, “WHAT DO THEY MEAN” BONYEZA HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments